Wednesday, February 01, 2006

Salaamu kwa Wanablogu.

Asalaam alaikum ndugu zangu wananblogu!.Kama nilivyodokeza hapo jana ni kwamba nitakuwa nikiwaletea au nikiwadondoshea matone ya fikira kutoka katika kisima hiki ambacho kimechimbwa masaa kadhaa yaliyopita.Kama ilivyo jadi ya wanablogu kama Makene, Minja, Mwaipopo na Ndesanjo amabaye jitihada zake kuhakikisha vijana nasi tunakuwa "bloggerised",kama wenzetu hawa wenye ung'eng'e wanavyoweza kusema namshukuru sana kwani ameamsha baragumu.Baragumu nalo baada ya kupiga kwa mda mrefu kiu ikalikamata ikabidi nalo litafute kisima ili nacho kitowe maji ya kulainisha koo.Kwa mantiki hiyo basi, ni maji hayo hayo yatakayolainisha akili hasa za watanzania wenzetu waliolala ili waweze kufahamu yanayojili nje ya bongo kupitia blogu hizi.Nawaomba muendelee kuwapatia wenye kiu kisima hiki wakati huu wa ukame.Nawahi kuingia darasani nitawapasha habari zingine hapo baadaye.

4 Comments:

At 3:58 AM, Blogger Innocent said...

Nakukaribisha sana.Nataraji nitajifunza mengi kutoka kwako kama itakavyokuwa kwangu pia.
Kwa ufupi usikose kusoma globu yangu kutoka Uganda.

 
At 9:15 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Haya sisi tunasubiri hayo maji sijui yatazaa togwa au itakuwa chang'aa.

 
At 2:18 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Kisima cha weledi hakika umekuja na staili njema kabisa. Mie nilipata taabu sana kuanza kutumbukiza picha ndani ya blogu. Wewe si haba. Basi kasi, ari na nguvu sio tu viwe vipya bali viwe chachu ya mabadiliko chanya. Kule Bongo nasikia sasa kila kitu ni kwa kasi, nguvu na ari mpya: ulevi, ujambazi, rushwa, watoto kukosa nafasi za kwenda fomu wani nk (nimesoma magazetini).

Karibu na ujisikie u-huru.

 
At 3:40 AM, Blogger Indya Nkya said...

Karibu kaka. Tupo wote

 

Post a Comment

<< Home