Sunday, February 05, 2006

Mnyama Msumbufu.

Je, Unamfahamu mnyama msumbufu? Majawabu mbali mbali yaweza kutolewa yupi ni mnyama msumbufu kuliko wote hasa kwa wale wafugwao.Jibu la haraka mtu aweza kusema ni mbuzi kwa wale waliowahi kukaa vijijini wakakumbana na shughuli za kuchunga mnyama huyu wanalifahamu vizuri hilo. Anajulikana kama mbuzi japokuwa ndugu yangu Mwaipopo kwao anajulikana kama mbusi.Kwa wale "maboni tawuni", nasema kumradhi sana kwani mtakuwa hamuelewi purukushani za huyu mnyama isipokuwa mnamfahamu katika mahadhi ya kimapishi hasa kupitia kitoweo chake muruwa.
Kwa upande mwingine binadamu kama kiumbe alipewa uwezo na akili za utashi ni kiumbe msumbufu kuliko vyote.Pamoja na akili yake, kiumbe huyu haridhiki na kila hali aliyonayo.Nikianzia na mimi nilipokuwa Dar es Salaam nilikuwa nalalamika joto na kulala bila hata kujifunika.Hali hii ilisababisha malalamiko makubwa sana kiasi kwamba hata wakati mwingine nilisahau kwamba mambo haya ni ya asili na kuna mtu aliye na nguvu za kufanya marekebisho na hivyo kukufuru mda wote.Hamadi nikapata hii fursa ya kuja huku Steti kama panavyojulikana kule bongo kwa kupatukuza.Wakaniambia nitakuta baridi kali hadi barafu nikasema itakuwa vizuri manake hili juwa lilikuwa linakaribia kunitowa roho.Nilipotuwa huku tabu ikaanza mwanetu mimi nimeonea wapi barafu nchi kavu!Malalamiko yakaanza.Baridi imezidi maisha yangu yako hatarini.Wenyeji wkaniambia hujaona baridi bado!Ipo inakuja na utasimulia hadi vizazi vyako.Nikasema , "Nfwile mwana gwa kyala".Hapo binadamu nikaonekana kumsumbuwa aliyenijalia kuja huku.
Katika hali nyingine ya kushangaza wapendwa wanablogu, nikwamba mnajuwa kuwa bongo imekumbwa na janga la ukame ulioambatana na njaa.Ukame huu umesababisha matatizo makubwa sana kama ukosefu wa chakula cha kutosha na umeme wa mgawo ambao kama ndugu yangu Makene na Lubuva wangekuwepo ingekuwa patashika nguo kuchanika. Hali hii ya ukame iliwapa watu wa kila aina mchecheto hasa ukizingatia njaa ndiyo ilikuwa inatesa jamii kila upande wa nchi.Ni juzi tu watu walikusanyika pale VIWANJAVYA JANGWANI kumuomba Mwenyezi Mungu awajaalie mvua.Cha kushangaza mvua imeanza kunyesha kwa staili ya viroba na sasa binadamu msumbufu kaanza kulalamika kwamba mafuriko yamezikosesha familia makazi huko Tabora.Ewe binadamu kiumbe msumbufu usiyeridhika, kipi bora jua au mvua?

3 Comments:

At 5:19 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Kisima: tunatamka 'mbusi' pale tunapojifunza Kiswahili lakini jina halisi la mnyama huyo kwa Kinyakyusa ni 'mbene'

 
At 4:23 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Wanadamu!
Nashangaa sana wanadamu tunapoharibu mfumo wa asili wa kuleta majira (ikiwemo mvua). Kisha tunakwenda kusali ili mungu alete mvua. Kama mvua inaletwa kwa sala, mbona basi jangwani hakuna mvua? Ina maana kuwa wanaoishi majangwani hawasali?

 
At 11:27 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Swali zuri sana Ndesanjo

 

Post a Comment

<< Home