Thursday, February 02, 2006

Mbinu Mpya ya Majambazi Tanzania.

Katika hali ya kustaajabisha, watu wamebaki wamejishika tama huku wakijiuliza kulikoni ndani ya serikali hii iliyoingia na falsafa ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Ikumbukwe kwamba falsafa za namna hii zimekuwa kama kichocheo cha uharifu ndani ya jamii zikiwa zimeanzishwa na viongozi wanaoingia madarakani au wanaotaka kuingia madarakani. Ni awamu iliyopita tu ya braza Benny iliingia na "mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe". Na baada ya kitambo kidogo tu wasafiri wa mabasi kupitia Singida walivamiwa na majambazi na kuvuliwa nguo zao zote na kunyang'anywa kila kitu huku wakiimba, "mtaji wa Maskini ni nguvu zake mwenyewe".

Kwa kutafuta staili ya mtoko, JK naye akaona bora aandae falsafa yake ili aamushe hamasa miongoni mwa watanzania.Nakubali kwamba falsafa hizi zinatumiwa na mabwana hawa kwa nia nzuri, lakini watu walalahoi ambao wameona unyanganyi wa mali na roho za watu wasiokuwa na hatia ndiyo njia pekee ya kupambana na maisha ndani ya nchi inayopambana na janga la ukame na njaa.Sasa ni karibia matukio ya ujambazi ishirini yametokea, lakini lilotia fora ni lile la jana la NBC Bank pale karibu na Ubungo Plaza.Unajuwa ni mbinu gani iliyotumika?Ngoja nikusimulie kisa kilivyoanza.

Kama kawaida benki ni sehemu ambapo kila mtu anakwenda kuweka fedha yake au kuchukuwa fadha yake kwa matumizi mbalimbali.Wote tunalifahamu hilo na zaidi ya yote hata watu waweza kwenda pale kuomba mikopo ya kaanzishia biashara zao.Kuweka hela benki kwaweza kuwa ni sababu ya kiusalama, kuzibiti matumizi kwa watu wanaowashwa na fedha pindi ikiwa mfukoni na kupata riba kwa wengine. Kabla sijaenda mbali, kwanza ngoja niwarejeshe kwenye mbinu hiyo iliyokwapua mamilioni ya madafu yasiyofahamika idada yake na kutokomea hivi huku raia wakiona ni sinema ya "Holiwudi".Mbinu hiyo ni ya kishehe au Kiimamu,wale maswahiba wenzangu mwaweza kuwa mnawafahamu yakhe!Ni kwamba majamaa yaliingia na kanzu zao zilizopambwa na baraghashia utafikri yanatinga masjidi.Hii ni kali.Labda hapo baadaye yatamwiga padri au askofu.Ni katika hali hiyo bila kutegemea wateja wakaona gauni zile zimejifunguwa ghafla bini vu siraha za kila aina bastola, SMG n.k. Sasa hapo kilichofuta ni kusalimisha kilicho chao kama unataka uendelee kuvuta hii hewa na kusubiria kifo kilichopangwa na Allah.Ni katika hali hiyo pia majambazi hawa kwakatokea kama chui waliovaa ngozi ya chui kutawafanya vijana wa Mahita washindwe kuwadhibiti.

Mimi ni msomaje mzuri sana wa magazeti ya bongo kila siku.Lakini nilipopitia gazeti moja na kuona Mahita akitetea unga wake kwa kusema sasa vijana wake inabidi wazame striti ili wapambane na vijana wanaoiba kwa kutumia falsafa ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Mimi nilitamani watu wangempa mawazo huyu mzee namna ya kuwaimarisha hawa vijana wake. Jeshi la polisi linatakiwa kupewa elimu ya haki za binadamu pamoja na mbinu mpya za kupambana na uharifu. Nikimaanisha wajifunze zaidi nini wanachotakiwa kufanya ili kuondoa tatizo hilo sugu la ujambazi. Na vile vile wapewe siraha kubwa hasa maeneo ya taasisi za kifedha badala ya kukaa na virungu. Wajifunze namna ya kutafuta habari za majambazi hao ili wazuwia uharifu unaoweza kujitokeza.Hapa mbinu mpya zinatakiwa ziimarishwe pande zote za nchi hasa Dar.Kwa hali inayoonekana kukerwa na ujambazi, Mwamnyange naye kaja na njia nyingine ya kiini macho ati kufanya msako nchi nzima wa siraha zinazomilikiwa kiharamu.Kama inatangazwa kwamba watafanya msako wanafikiri wamiliki ni wajinga?Watahakikisha wamezificha zana zao za kazi.Napenda kuhitimisha kwa kuwataka wabongo wenzangu wawe macho pengine njia ya unabii hapo baadaye yaweza kutumika kuiba na hivyo kubaki swala la imani au kuabudu kukiwa ni tishio. Asalaam alaikum waallah matulallah wabaallahkatuh!

5 Comments:

At 2:33 AM, Blogger mwandani said...

Majambazi mbona wanatufanyia masihara lakini? imekuwa kila ukisoma gazeti pana tukio. Siamini ati nchi nzima, serikali yote haina jawabu!

 
At 4:30 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kuna wizara mbili hivi sasa ambazo zina jukumu la kuhakikisha usalama wa raia lakini ndio kwanza majambazi wanafanya wanachotaka. Kwangu mimi, pamoja na kuwa tatizo ya ujambazi ni ishara ya uozo wa rushwa, uongozi lelemama, n.k., hii ni ishara ya hatua ambayo taifa limefikia kiuchumi na kijamii.

 
At 9:21 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Ndesanjo suala si matanuzi ya wizara. Hoja ni je kuna uwiano katika utendaji na kuna kuthubutu kufanya yale ambayo umeahidi kusimamia. Kinachoogopwa ni nini au kuna wakubwa wananufaika na suala hili moja kwa moja?

 
At 7:07 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kisima,
Nimemaliza kuandika makala ambayo nimekunukuu na pia kuweka anuani ya blogu yako. Kila ninapomnukuu mwanablogu siku hizi ninaweka anuani ikiwa ni moja ya njia ya kuwezesha watu wengi zaidi kusoma blogu zetu.

 
At 12:44 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Kisima hongera kwa kuchambua mbinu hizi za kianaizaya zilizobuniwa na wandugu wachache ambao hawapendi kuzihusisha bongo zao kutafuta mapato halali. Shafi Adam Shafi aliyeandika kitabu cha Kuli aliandika 'Yana Mwisho haya'. Basi mwisho wake utaletwa na changamoto tunazozipata katika visima, makasri, mamwandani, ma-Da'mija, mandesanjo, majeff na 'kazalika'

 

Post a Comment

<< Home