Tuesday, January 31, 2006

Hala Hala Naja Bloguni


Nimekuwa nikisikia blogu na kelele nyingi zikija masikioni mwangu kuhusu huyu blogu ila sikuwa na shauku ya kuwa nayo.Hala hala sasa naja kwa kishindo nkitokea ndani ya barafu inayokaribia kunigandisha mapafu.Halafu kitu kingine kilichonizuwia ilikuwa ni staili ya kutoka na blogu hilo.Kelele za ndugu yangu Makene na Mnyambala Mwaipopo hatimaye zimefanikisha jukumu la uwanja wa pekee kuwapa mawazo.Haya karibuni tubadilishane mawazo kwa njia hii yenye uhuru wa kipekee.
Katika picha hiyo naonekana upande wa kushoto nyuma nikiwa nimevaa fulana nyeusi. Waliosimama kutoka nyuma na waliokaa kutoka kushoto ni Subira Kabula, Makene Boniphace na Clara Francis bila kumsahau mnyambala mwenzangu kutoka Mbeya tuliyesimama naye nyuma kwenye picha.Hawa wote ni walimu wa Kiswahili katika vyuo vikuu mbali mabali huku Marekani.

11 Comments:

At 9:46 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Karibu sana Kisima cha Weledi. Tunatarajia kupata maji ya liwazo ya fikra katika kisima chako na tunaamini utakuwa mkarimu kwa wote watakaohitaji huduma ya maji ya fikra toka kisimani kwako. Nimepita na kukuweka kwangu pale ili wasomaji wangu nao wapate fursa ya kukutembelea hapa. Mark Msaki upoooo.

 
At 10:26 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Hala hala zako tumezipata nasi tunakaa chonjo. Naomba unifikishie ujumbe wangu kwa Kina Da'Subira Kabula na Clara Francis kwamba nao tunawasubiri kwa hamu.

Karibu sana.

 
At 11:03 AM, Blogger Boniphace Makene said...

uSIJALI HAWA WANAKUJA BAADA YA SIKU CHACHE, mija lakini mbona swali langu nililokuachia pale kwa Michuzi hukujibu?

 
At 11:45 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Bado ninalikumbuka sema tu nimetingwa kidogo, lakini nitalijibu hivi karibuni. Vuta subira.

 
At 12:18 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Karibu mwanakwetu Januari. Si shaka sasa umepata kisemeo pepe cha dukuduku na maoni yako, nasi basi tuweze kuzima kiu zetu.

Da'Mija: swali la Kasrilamwanazuo haliitaji kuwa profesa hata kufikiri saaaana. Ni vema ukakata kiu yake sasa hivi kulikp baadaye.

Wengine woote: Matatizo ya kiufundi yananifanya nisipatikane mara kwa mara. Yawezekana mwapata taabu kunifikia au hamnifikii kabisa. Utatuzi u njiani kuja sasa hivi kuliko baadaye.

 
At 4:53 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Januari,
Karibu sana.Umeanza vizuri na ninaomba uendelee hivyo hivyo.Uzuri wa hapa,hakuna atakayekufunga gavana.Karibu sana.

 
At 10:41 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Namuunga Mkono Da Mija: akina Da Subira na Clara nao waje tuhangaike nao.

Halafu hili swali mnaloongelea kuwa kaulizwa Da Mija ndio swali gani hilo?

 
At 10:42 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kisima Weledi,njoo. Karibu. Karibu hadi ndani. Tumetoka mbali. Toka enzi za habari kuwa lazima zipitie Shihata hadi leo hii ambapo mimi na wewe tuna "shihata" yetu bila kuomba ruhusa kwa kiumbe yeyote yule. Safari ndefu. Nimefurahi sana kupata habari toka kwa Makene kuwa tuna wageni.

 
At 2:07 AM, Blogger mark msaki said...

karibu sana kisima cha Weledi. ni fahari kubwa wanablogu wa kiswahili tunapopata mapioneer ambao ni wataalamu wa lugha yetu..tunaamini sasa hata ile kiu ya kupata maana ya neno blogu kwa kiswahili itatimia, wachilia mbali masuala mengine ya kiufundi...mfano ni nini maana ya pioneer kwa kiswahili?

amini usiamini, blogu itakufundisha, itakupa nafasi ya kufundisha, itakuonyesha dunia inapokwenda, na itakuruhusu kuwa raia anayefaa wa nchi yetu na dunia kwa ujumla..itakushauri ufanye nini ili uwe mtumishi bora wa raia wa mungu!!

 
At 8:55 AM, Blogger mloyi said...

Umekuja kama Januari
Mwezi wa kwanza wa mwaka
Wa mwisho hukuanzia
Jioni timiza.

Kisima kimeingia kisikauke matoleo, tunahamu ya kukichota hadi tuishe.

 
At 3:22 AM, Blogger Walter Macha said...

Karibu sana.Ingawa mimi sijaanza kublogu huwa napenda kukaribisha watu kwenye blogu na kusoma maoni yao.

 

Post a Comment

<< Home